08 November 2012
LEO NIMEIONA HASIRA YA MUNGU LIVE.
Leo nilikua safarini kuelekea ARUSHA mji ambao siwezi ku usahau maishani mwangu kutokana na historia kubwa nliyo nayo na mji huo. Safari yangu niliianza asubuhi na mapema sana na nilitegemea kuwasili mapema kabla jua halijachwa. Hua nikisafiri natamani sana kukaa siti moja na mzee au binti tunaelingana nae kwa umri na sababu ya mapenzi yangu hayo ni nzuri wala si ya kuhofia; kwa bahati mbaya leo nilikaa na kijana wa kiume wa miaka thelathini na zaidi hivi. Bwana huyu alinistua kwani alikua anabishana na konda tangu alipokua anakuja na alipo kaa tu chini aliporomosha MATUSI mazito yaliyofanya abiria wote kua kimya ghafla,moyoni nilijisemea mwenyewe kua leo nimepatikana ...
Safari yetu ilinza kama kawaida na tulipofika maeneo ya MBEZI KIMARA, alipanda kijana mmoja mwenye sura ya upole, akiwa ameshikilia BIBILIA MKONONI na aliitusalimia kwa ustaarabu akajitambulisha kisha akafungua Bibilia yake akaisoma "KILA ATENDAYE DHAMBI ,AFANYA UASI; KWA KUA DHAMBI NI UASI" .alipo maliza kusoma yule jirani yangu akanisemesha " HAWA HUA WANATAKA HELA TU" nilitabasamu na kuendelea kukaa kimya. akaendelea tena kuongea tena kwa sauti " OYA NJOO UCHUKUE HELA UTUACHIE KELELE SISI" baadhi ya watu waliaangua kicheko lakini yule mhubiri aliendelea kuhubiri.Alipo maliza kuhubiri akatuombea kisha kweli kama kawaida alialika watu kutoa sadaka. waliojaliwa walitoa na yule jirani yangu aalimuita yule muhubiri huku akinyoosha noti ya elfu kumi. Alipo kuja sikuamini macho yangu kwani alimchapa kibao cha ghafla kisha akamwambia "mimi nlikuambia UJE UCHUKUE HELA UTUACHIE KELELE KWA NINI ULIKATAA? " Wakati yule kijana amebaki ameduwaa yule bwana akamtwanga kibao kingine usoni ,sikua na lakufanya ila baadhi ya abiria na konda walikuja na kuamsha mzozo. Sijui yule BWANA alikua anajiaminin kwa kitu gani alianza kutukana na hatimaye abiria walishauri twende polisi .
Gari liliendelea na safari kuelekea poliisi huku mzozo kati ya baadhi ya abiria na yule jirani yangu ukiendelea. Tuliingia polisi na yule bwana alishushwa. Wakati wanaelekea kituoni BODA BODA ILITOKEA GHAFLA NA KU MGONGA YEYE PEKE YAKE.. ALIANGUKA CHINI NA KWA KUA NILIKUA DIRISHANI NILISHUHUDIA ULE MKANDA LIVE.. TULIBAKI KUSHANGAA NA MASWALI MENGI YASIYO NA MAJIBU SAHIHI YALIJAZA VICHWA VYETU ..;NILIJISEMEA MOYONI LEO NIMEIONA HASIRA YA MUNGU LIVE..